عن جندب بن عبد الله رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَنْ صَلَّى صلاةَ الصُّبْحِ فهو في ذِمَّةِ اللهِ فلا يَطْلُبَنَّكُمُ اللهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ، فَإِنَّهُ مَنْ يَطْلُبْهُ مِنْ ذِمَّتِهِ بِشَيْءٍ يُدْرِكْهُ، ثُمَّ يَكُبُّهُ على وَجْهِهِ في نَارِ جَهَنَّمَ».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jundub bin Abdallah Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Atakaye swali swala ya Al-fajiri atakuwa katika mkataba wa Mwenyezi Mungu, hivyo asikutafuteni Mwenyezi Mungu katika mkataba wake kwa chochote, kwani mwenye kumtafuta katika mkataba wake kwa chochote basi humpata, kisha humuinamisha uso wake katika moto wa Jahannamu".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Atakaye swali swala ya subuhi basi atakuwa kaingia katika mkataba wa Mwenyezi Mungu, anakuwa ni kama vile kaandikishana na Mwenyezi Mungu kuwa asidhuriwe na yeyote, hivyo hatakiwi kuudhiwa kutoka kwa yeyote; kwasababu kumuudhi kwake kiuhalisia inazingatiwa kuwa ni kumfanyia uadui Mwenyezi Mungu na ni kuvuruga amani yake ambayo kampa zawadi huyu mwenye kuswali, na atakayevunja mkataba wa Mwenyezi Mungu na akaufanyia uadui atakuwa kaiingiza nafsi yake katika kupambana na Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humlipizia kisasi aliyeudhiwa haliyakuwa yuko pembezoni mwake na amani yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kubainishwa kwa umuhimu wa swala ya Al-fajiri na ubora wake.
  2. Tahadhari kubwa ya kumfanyia ubaya mwenye kuswali swala ya subuhi.
  3. Kuhifadhi mipaka ya Mwenyezi Mungu na makatazo yake ni sababu ya Mwenyezi Mungu kumhifadhi mja na kumsaidia.