عن جرير بن عبد الله رضي الله عنه قال: بَايَعْتُ رسول الله صلى الله عليه وسلم على إِقَام الصَّلاَة، وإِيتَاء الزَّكَاة، والنُّصح لِكُلِّ مُسلم.
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jariri bin Abdillahi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Nilimpa utiifu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kumnasihi kila muislamu.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Amesema Jariri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Nilimpa utiifu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kumnasihi kila muislamu, na kumpa utiifu hapa inamaana ya kumpa ahadi, na imeitwa hivyo hapa kwasababu kila mtu katika hawa wanaoingia makubaliano hunyoosha mkono kwa mwenzie, yaani mkono wake kwaajili ya kushika mkono wa mwenzie, na haya ni mambo matatu: 1- Haki halisia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu . 2- Haki halisia ya mwanadamu 3- Haki ya pande zote. Na ama haki halisia ya Mwenyezi Mungu, ni kauli yake: "kusimamisha swala" yaani ailete muislamu ikiwa imenyooka kwa namna inayotakiwa, aihifadhi kwa wakati wake, na atekeleze nguzo zake na wajibu wake na sharti zake, na aikamilishe hiyo kwa mambo yake ya sunna. Na inaingia katika kusimamisha swala upande wa wanaume kusimamisha swala msikitini pamoja na jamaa, kwani hili ni katika kusimamisha swala, na katika kusimamisha swala pia: Ni kuwa na unyenyekevu ndani yake, na unyenyekevu ni kunyenyekea kwa moyo katika yale anayoyasema mwenye kuswali na anayoyafanya, nalo ni jambo muhimu; kwani ndiyo moyo wa swala na roho yake. Na ama jambo la tatu: -Ambalo ni haki ya pande zote ni kauli yake: "Kutoa zaka": Yaani kuitoa kumpa mwenye kustahiki. Na ama jambo la pili: -Ambalo ni haki ya mwanadamu- ni kauli yake: "Ni kumnasihi kila muislamu", Yaani nasaha kwa kila muislamu: wa karibu au wa mbali, mkubwa au mdogo, mwanaume au mwanamke. Na namna ya kumnasihi kila muislamu ni ile aliyoitaja katika hadithi ya Anas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- "Hawezi kuamini mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake yale anayoyapendelea nafsi yake" hii ndiyo maana ya nasaha, uwapendelee ndugu zako yale unayoyapendelea nafsi yako, yakufurahishe yale yanayowafurahisha, na yakuchukize yanayowachukiza, na uwafanyie yale unayopenda na wao wakufanyie, na mlango huu ni mpana na ni mkubwa sana.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama