عَنْ حُذَيْفَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
كُنَّا إِذَا حَضَرْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَعَامًا لَمْ نَضَعْ أَيْدِيَنَا حَتَّى يَبْدَأَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَيَضَعَ يَدَهُ، وَإِنَّا حَضَرْنَا مَعَهُ مَرَّةً طَعَامًا، فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ كَأَنَّهَا تُدْفَعُ، فَذَهَبَتْ لِتَضَعَ يَدَهَا فِي الطَّعَامِ، فَأَخَذَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِهَا، ثُمَّ جَاءَ أَعْرَابِيٌّ كَأَنَّمَا يُدْفَعُ فَأَخَذَ بِيَدِهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ الشَّيْطَانَ يَسْتَحِلُّ الطَّعَامَ أَنْ لَا يُذْكَرَ اسْمُ اللهِ عَلَيْهِ، وَإِنَّهُ جَاءَ بِهَذِهِ الْجَارِيَةِ لِيَسْتَحِلَّ بِهَا فَأَخَذْتُ بِيَدِهَا، فَجَاءَ بِهَذَا الْأَعْرَابِيِّ لِيَسْتَحِلَّ بِهِ فَأَخَذْتُ بِيَدِهِ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنَّ يَدَهُ فِي يَدِي مَعَ يَدِهَا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2017]
المزيــد ...
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hatuweki mikono yetu mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi anaweka mkono wake, na hakika sisi kuna wakati tulihudhuria chakula pamoja naye, akaja kijakazi kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akamshika mkono wake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho, na bila shaka alikuja na kijakazi huyu ili akihalalishe, nikashika mkono wake, akaja tena na Bedui huyu ili akihalalishe nikamshika mkono, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wake umekamatwa na mkononi wangu pamoja na mkono wake kijakazi".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2017]
Ameeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.