عن معاذ بن جبل رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «يَا مُعَاذ، واللهِ، إِنِّي لَأُحِبُّكَ، ثُمَّ أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ، لاَ تَدَعَنَّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاَة تَقُول: اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ، وَشُكْرِكَ، وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي ومالك وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Mu'adhi bin Jabali -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Alisema: "Ewe Mu'adhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda, kisha ninakuusia ewe Mu'adhi, hakikisha usiache mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainniy alaa dhikirika -Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mimi juu ya kukutaja wewe, Washukurika- na kukushukuru, Wahusni ibaadatika -Na kuzifanya vizuri ibada zako".
Sahihi - Imepokelewa na An-Nasaaiy

Ufafanuzi

Inatupa picha hadithi ya Mu'adhi ya nembo mpya katika nembo za mapenzi ya kiislamu, ambayo katika matunda yake ni nasaha na muongozo katika kheri, kwasababu Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alisema kumwambia Mu'adhi "Hakika mimi ninakupenda" na akaapa akasema: "Wallahi hakika mimi ninakupenda" na hii ni nafasi kubwa kwa Mu'adhi bin Jabali -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- aliapa kuwa hakika yeye anampenda, na mpenzi huwa hawekezi kwa ampendaye isipokuwa yale yaliyo na kheri kwake; bali alisema haya kumwambia; ili ajiandae kupokea yale atakayomueleza; kwasababu anayatoa kumpa ampendaye. kisha akasema kumwambia: "Hakikisha usiache kusema kila baada ya swala" Yaani ya faradhi, Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie mimi juu ya kukutaja wewe na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako": Na mwisho wa kila swala yaani: mwisho wa swala kabla ya kutoa salamu, hivi ndivyo ilivyokuja katika baadhi ya riwaya, kuwa yeye aseme kabla ya salamu na ndio haki, na kama ilivyokuja kuwa neno nyuma, yaani nyuma ya swala, ikiwa ni dua basi hiyo itakuwa kabla ya salamu, na kama dhikiri yaani uradi basi hiyo inakuwa baada ya salamu, na inaonyesha hilo katika msingi huu nikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alisema katika hadithi ya bin Mas'udi katika tahiyatu alipoieleza akasema: kisha mtu achague katika dua kile anachokitaka au kile anachokipenda na kikampendeza, na ama dhikiri amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: -"Pindi mnapomaliza swala basi mtajeni Mwenyezi Mungu kwa kusimama au kwa kukaa na mkiwa mmelala". Na kauli yake: "Nisaidie mimi juu ya kukutaja wewe" Yaani: kila kauli inayoleta ukaribu kwa Mwenyezi Mungu, na kila kitu kinacholeta ukaribu kwa Mwenyezi Mungu, basi hicho kiko katika kumtaja yeye na kumshukuru yeye, Yaani: kushukuru neema na kuondolewa adhabu, ni neema ngapi za Mwenyezi Mungu ziko kwa viumbe wake, na ni adhabu ngapi zilizoondoshwa kwao; akamshukuru Mwenyezi Mungu juu ya hilo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama
Ziada