+ -

عَنِ ‌ابْنِ أَبِي أَوْفَى رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا رَفَعَ ظَهْرَهُ مِنَ الرُّكُوعِ قَالَ: «سَمِعَ اللهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، اللَّهُمَّ رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ، مِلْءَ السَّمَاوَاتِ وَمِلْءَ الْأَرْضِ وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 476]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 476]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuuu ndani ya swala, anasema: " Sami'allaahu liman hamidah", Yaani: Atakayemhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamjibu, na atakubali himidi zake na atamlipa, kisha atamhimidi kwa kusema: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati, wamil al Adhwi wamil amaa shi ita min shai in baad", himdi zenye kujaza mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, na zinajaza ayatakayo Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa anayotakiwa kusema mwenye kusali anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu.
  2. Sheria ya kulingana sawa na utulivu baada ya kuinuka kutoka katika rukuu; kwa sababu haiwezekani aseme dhikiri hii ila baada ya kusimama wima na kutulia.
  3. Dhikiri hii ni sheria katika swala zote, sawa sawa ziwe za faradhi au za sunna.