عَنْ ‌وَرَّادٍ كَاتِبِ الْمُغِيرَةِ بْنِ شُعْبَةَ قَالَ: أَمْلَى عَلَيَّ الْمُغِيرَةُ بْنُ شُعْبَةَ فِي كِتَابٍ إِلَى مُعَاوِيَةَ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ: «لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لَا مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلَا مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلَا يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ».

[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Warraadi mwandishi wa Mughira amesema: Alinisomea Mughira bin Shu'ba katika kitabu kilichoandikwa kwenda kwa Muawia:
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikua akisema mwishoni mwa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu".

Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema kabla kidogo ya mwisho wa kila swala ya faradhi: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu laa shariika lahu, lahul mulku walahul hamdu, wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Allaahumma laa maania limaa a'twaita walaa mu'twiya limaa mana'ta, walaa yanfa'u dhal jaddi minkal jaddu"
Yaani: Nina kiri na kulikubali neno la kumpwekesha Allah, la Laa ilaaha illa llaah, -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah-, ibada ya kweli naithibitisha kwa Mwenyezi Mungu, na ninaikanusha kwa asiyekuwa yeye, hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Allah, na ninakiri kuwa ufalme wa kweli uliotimia ni wa Mwenyezi Mungu, na sifa zote za viumbe wa mbinguni na ardhini zinamstahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu, kiasi kwamba yeye ndiye muweza juu ya kila kitu, na aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu katika vipawa au kunyimwa hakuna awezaye kuyazuia, na hapo basi utajiri hauwezi kumsaidia mwenye nao, bali kinachoweza kumfaa ni amali zake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kupendeza kusomwa dua hii mwisho wa swala kwakuwa imekusanya lafudhi za tauhidi na himdi.
  2. Kufanya haraka kuitekeleza sunna, na kuitangaza.
Ziada