عن حُذَيْفَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَقُولُ بَيْنَ السَّجْدَتَيْنِ: «رَبِّ اغْفِرْ لِي، رَبِّ اغْفِرْ لِي».

[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن ابن ماجه: 897]
المزيــد ...

Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema kati ya sijida mbiliL "Rabbigh-firlii, Rabbigh-firlii".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abu Daud, Nasai, Ibn Majah na Ahmad] - [Sunanu Ibn Maajah - 897]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema wakati wa kikao kilichopo baina ya sijida mbili: Rabbigh-firlii, Rabbigh-firlii.
Na maana ya Rabbigh-firlii: Ni mja kuomba kutoka kwa Mola wake ayafute madhambi yake na asitiri aibu zake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya dua hii kati ya sijida mbili katika swala ya faradhi na sunna.
  2. Inapendeza kuirudiarudia kauli ya Rabbigh-firlii, ila wajibu ni kuisema mara moja.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (58)