عن عُثْمَانَ بْنَ أَبِي الْعَاصِ رضي الله عنه:
أنه أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ حَالَ بَيْنِي وَبَيْنَ صَلَاتِي وَقِرَاءَتِي يَلْبِسُهَا عَلَيَّ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «ذَاكَ شَيْطَانٌ يُقَالُ لَهُ خِنْزَِبٌ، فَإِذَا أَحْسَسْتَهُ فَتَعَوَّذْ بِاللهِ مِنْهُ، وَاتْفُلْ عَلَى يَسَارِكَ ثَلَاثًا»، قَالَ: فَفَعَلْتُ ذَلِكَ فَأَذْهَبَهُ اللهُ عَنِّي.
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2203]
المزيــد ...
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake-:
Yakwamba yeye alimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika shetani amekaa kati yangu na swala yangu na kisomo changu ananichanganya, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu", anasema: Nikafanya hivyo Mwenyezi Mungu akamuondosha kwangu.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2203]
Alikuja Othman bin Abil Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yake- kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika Shetani ameziba kati yangu na swala yangu, na amenizuilia na kupata utulivu ndani yake, na amenichanganyia kisomo changu na amenitia wasi wasi ndani yake, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Huyo ni Shetani aitwaye Khinzab, ukihisi hali hii basi taka kinga kwa Allah, na utake ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme mate kushotoni kwako mara tatu, Othman anasema: Nikafanya aliyoniamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Mwenyezi Mungu akaniondolea hali hiyo.