عَن ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما:
أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَرْفَعُ يَدَيْهِ حَذْوَ مَنْكِبَيْهِ إِذَا افْتَتَحَ الصَّلَاةَ، وَإِذَا كَبَّرَ لِلرُّكُوعِ، وَإِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ مِنَ الرُّكُوعِ، رَفَعَهُمَا كَذَلِكَ أَيْضًا، وَقَالَ: «سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، رَبَّنَا وَلَكَ الحَمْدُ»، وَكَانَ لاَ يَفْعَلُ ذَلِكَ فِي السُّجُودِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 735]
المزيــد ...
Na kutoka kwa Ibn Omari Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake:
Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akinyanyua mikono yake usawa wa mabega yake anapofungua swala, na anapotoa takbira ya kurukuu, na anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anainyanyua pia, na akasema: "Sami'a llaahu liman hamidahu" Yaani: Amemsikia Mwenyezi Mungu yule aliyemuhimidi, "Rabbanaa walakal hamdu" Mola wetu Mlezi na sifa njema ni zako, na alikuwa hafanyi hivyo katika sijida.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 735]
Mtume, rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akinyanyua mikono yake katika sehemu tatu wakati wa kuswali, usawa wa mabega ni: Pale panapounga kati ya mfupa wa bega na mkono.
Sehemu ya kwanza: Anapofungua swala wakati wa takbira ya kuhirimia swala.
Sehemu ya pili: Anapotoa takbira kwa ajili ya rukuu.
Sehemu ya tatu: Anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu, na akasema: Sami'allahu liman hamidah, Rabbanaa walakal hamdu. Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi, Mola wetu Mlezi, na sifa njema ni zako.
Na alikuwa hanyanyui mikono yake wakati wa kuanza kusujudu, wala wakati wa kunyanyua kutoka katika sijida.