عن عبد الله بن مَسْعُود رضي الله عنه قال: عَلَّمَنِي رسول الله صلى الله عليه وسلم التَّشَهُّد، كَفِّي بين كفيه، كما يُعَلِّمُنِي السورة من القرآن: التَّحِيَّاتُ للَّه، وَالصَّلَوَاتُ وَالطَّيِّبَاتُ، السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته، السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أن محمدا عبده ورسوله». وفي لفظ: «إذا قعد أحدكم في الصلاة فليقل: التحيات لله...» وذكره، وفيه: «فإنكم إذا فعلتم ذلك فقد سَلَّمْتُمْ على كل عبد صالح في السماء والأرض ...» وفيه: « ... فَلْيَتَخَيَّرْ من المسألة ما شاء».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Alinifundisha mimi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- tashahudi (tahiyatu), mkono wangu ukiwa katikati ya mikono yake kama anavyonifundisha sura katika Qur'ani: Attahiyyaatu lillaahi -Salamu ni za Mwenyezi Mungu- Wasswalawaatu wattwayyibaatu -Na swala na vilivyo vizuri- Assalaamu a'laika -Amani iwe juu yake- Ayyuhan nabiyyu- Ewe Nabii- Warahmatullaahi wabarakaatuh -Na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake- Assalaamu a'lainaa - Amani iwe juu yetu- wa a'laa i'baadillaahi sswaalihiin -na juu ya waja wema wa Mwenyezi Mungu, Ash-hadu an laa ilaaha illa llaahu -Ninashuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu- Wa ash-hadu anna Muhammadan a'bduhu warasuuluhu -Na ninashuhudia kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mjumbe wake-". Na katika lafudhi nyingine: "Atakapokaa mmoja wenu katika swala basi aseme: Attahiyyaatu lillaah" na akaitaja, na ndani ya lafudhi hiyo pia, "Kwani hakika nyinyi mkifanya hivyo mtakuwa mmemsalimia kila mja mwema mbinguni na ardhini" na dani ya lafudhi hiyo pia: "Basi mtu na achague katika maombi ayatakayo".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anaeleza Abdillahi bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alimfundisha tashahudi (tahiyatu) ambayo husemwa katika kikao cha swala cha kwanza na cha mwisho katika swala ya rakaa nne na tatu, na katika kikao cha mwisho katika swala ya rakaa mbili, Nakuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alitilia umuhimu wa kumfundisha tashahudi, akaweka mkono wake ndani ya mkono wake. Alianza na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu-, Kumtukuza kwa moja kwa moja, nakuwa yeye ndiye mwenye kustahiki swala na ibada zote, na vyote vizuri katika kauli na matendo na sifa. Na baada ya kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu akamsifia kwa kumuombea dua Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kusalimika na mapungufu na maafa, na akamuombea kwa Mwenyezi Mungu huruma na kheri, na ziada kamili juu yake, kisha akajiombea mwenyewe na waliopo katika wanadamu na Malaika. kisha akawajumuisha katika dua yake waja wote wa Mwenyezi Mungu wema, kuanzia watu, na majini, na Malaika wakazi wa mbinguni na ardhini na wenye kuwafuatia, na hii ni katika ufasaha wa kuzungumza kiujumla wa maneno yake -Rehema na Amani ziwe juu yake-. Kisha akashuhudia ushuhuda wa kweli yakuwa hapana aabudiwaye kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakwamba Muhammadi -Rehema na Amani ziwe juu yake- ana sifa mbili: Moja kati ya hizo: Nikuwa yeye anasifika na sifa ya uja (utumwa). Na ya pili: Ni sifa ya Utume. Na sifa zote mbili, ni sifa njema na tukufu, na ziko kati na kati, kati ya kuchupa mipaka na kutochupa mipaka. Na tashahudi (tahiyatu) imekuja kwa namna nyingi, lakini bora na maarufu kati ya zote ni tashahudi ya bin Mas'udi hii aliyoileta mtunzi, na inafaa pia kuleta namna zingine sahihi zilizobakia.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama