عن ابن عباس رضي الله عنهما أن النبي صلى الله عليه وسلم كان يقول بين السَّجدتَين: «اللَّهمَّ اغْفِرْ لي، وارْحَمْنِي، وعافِني، واهْدِني، وارزقْنِي».
[صحيح] - [رواه أبو داود]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Yakuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Alikuwa akisema kati ya sijida mbili: "Allaahumma ghfirlii, warhamnii, wa aafinii, wahdinii. warzuqnii (Ewe Mola wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya, na uniongoze, na uniruzuku)".
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Anaeleza bin Abbas Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- yakwamba, Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- "Alikuwa akisema kati ya sijida mbili: "Ewe Mola wangu nisamehe." Yaani: Alikuwa akiomba kati ya sijida mbili kwa dua hii, na hakuna tofauti kati ya swala ya faradhi na swala ya sunna, swala yote ni dhikri (kumtaja Mwenyezi Mungu) na kusoma Qur'ani, na maana ya kauli yake "Ewe Mola wangu nisamehe" Yaani: nisitiri, na usiniadhibu. "Na unirehemu" Yaani: nipe mimi toka kwako rehma zitakazokusanya kusitiri madhambi na kutoniadhibu, pamoja na kunipendelea kwa kunipa kheri mbili za dunia na Akhera. "Na unipe afya" Yaani: nipe amani na afya, katika dini yangu kutokana na makosa na mambo yenye kutatiza, na katika mwili wangu kutokana na maradhi na magonjwa, na katika akili yangu kutokana na uzezeta na wendawazimu, na maradhi makubwa ni maradhi ya moyo, ima kwa mambo yenye kutatiza yenye kupoteza, na ima kwa matamanio yenye kuangamiza, "Na uniongoze" Uongofu una aina mbili: Wa kwanza: Ni uongofu wa kujulisha na kuelekeza katika njia ya haki na kweli, na hili linapatikana kwa Muislamu na kafiri: Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: (Na ama watu wa thamud tuliwaongoza) [suratu fusswilat: 17], Yaani: tuliwaelekeza katika haki. Uongofu wa pili: Ni uongofu wa kuafikishwa (kuwezeshwa) na kukubali, na huu haupatikani ispokuwa kwa watu wenye imani, Na ndio unaotakiwa hapa: Niongoze katika haki na unidumishe juu yake. "Na uniruzuku" Yaani: nipe riziki, itakayonitosheleza katika maisha haya ya dunia na kuhitajia kwa viumbe wako, na unipe riziki pana Akhera, mfano wa ile uliyowaandalia waja wako wale uliowaneemesha.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kutulizana katika kikao kilicho kati ya sijida mbili, kama ilivyothibiti katika hadithi zingine pia.
  2. Uwajibu wa dua na kusema: Mola wangu nisamehe, Mola wangu nisamehe, kati ya sijida mbili.
  3. Kilicho bora ni alete dua kati ya sijida mbili kama ilivyokuja, ikiwa atazidisha au atapunguza katika hiyo haitobatilika swala yake.