عَنْ وَائِل بن حُجرٍ رضي الله عنه قَالَ:
صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَانَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ»، وَعَنْ شِمَالِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ».
[حسن] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 997]
المزيــد ...
Kutoka kwa Waili bin Hujari radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 997]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumaliza swala yake anatoa salaam kuliani kwake na kushotoni kwake kwa kugeuka kwa uso wake upande wa kulia, pamoja na kusema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na anatoa salaam kushotoni kwake, kwa kugeuza uso wake upande wa kushoto, pamoja na kusema: "Assalaam alaiku warahmatullah".