عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا سَجَدْتَ، فَضَعْ كَفَّيْكَ وَارْفَعْ مِرْفَقَيْكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 494]
المزيــد ...
Kutoka kwa Suhaib -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Utakaposujudu basi weka viganja vyako, na unyanyue viwiko vyako".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 494]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya mikono miwili katika sijida ya swala, nayo ni kwa kuviweka vizuri viganja vyake katika ardhi na aviweke vidole vikiwa vimefungamanishwa kuelekea kibla, na viwe viwiko viwili -maungio ya mkono na muundi wake- viwe vimenyanyuka na viko mbali na kugusa Ardhi, na vimeachanishwa na mbavu.