عن عبد الله بن الزبير -رضي الله تعالى عنهما- أنّه كانَ يقول: في دبر كل صلاة حين يُسلِّم «لا إله إلا الله وحده لا شريكَ له، له الملك وله الحمد وهو على كل شيءٍ قديرٌ، لا حولَ ولا قوةَ إلا بالله، لا إله إلا الله، ولا نعبد إلا إيَّاه، له النِّعمة وله الفضل، وله الثَّناء الحَسَن، لا إله إلا الله مخلصين له الدِّين ولو كَرِه الكافرون» وقال: «كان رسول الله صلى الله عليه وسلم يُهَلِّل بهن دُبُر كلِّ صلاة».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillaahi bin Zubair Radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwe juu yao- Ya kwamba alikuwa Anasema: kila mwisho wa swala anapotoa salamu: "Laa ilaaha illa llaahu wahdahu Laa shariika lahu, Lahul Mulku walahul Hamdu wahuwa a'laa kulli shai in qadiir, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah, walaa na'budu illaa iyyaahu, Lahun ni'matu walahul Fadhlu, walahuth thanaaul hasan, Laa ilaaha Illa llaahu Mukhliswiina lahud diina walau karihal kaafiruun" Yaani: Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, Ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, Hakuna ujanja wala nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, Na hakuna tunayemuabudu ila yeye, ana neema na ana fadhila, na ana sifa njema, Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu tunamtakasia dini hata kama makafiri watachukia" Na akasema: "Alikuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akimtukuza Mwenyezi Mungu kwa maneno haya kila mwisho wa swala".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Alikuwa Abdullahi bin Zubeir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- pindi anapotoa salamu katika swala za faradhi anasema utajo huu mtukufu, na ambao una maana nyingi sana tukufu, ikiwemo kuthibitisha uabudiwa wa kweli ni wa Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, na kukanusha kupatikana mshirika pamoja naye Mtukufu katika hilo, na kuthibitisha kupwekeka kwake kwa ufalme wa wazi na wa siri, na kustahiki kwake sifa kwa kila hali, na kuthibitisha uwezo wa moja kwa moja kwake Aliyetakasika na kutukuka, kama jinsi ilivyo ndani yake kuna kukiri mja kwa Mola juu ya kushindwa kwake na udhaifu wake, na kuwa kwake mbali na ujanja na nguvu na kukiri kwake kuwa hana ujanja wa kuweza kuzuia shari, wala hana nguvu za kuipata kheri ispokuwa kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama jinsi ilivyokusanya dhikri hii tukufu swala la kuziegemeza neema kwa mwenye kuzimiliki Aliyetakasika, na kuegemeza ukamilifu wa moja kwa moja na dhikiri tukufu na nzuri kwake yeye Aliyetakasika- juu ya dhati yake na sifa zake na vitendo vyake na katika kila hali, kisha ikahitimishwa dhikiri hii kwa neno la Tauhidi- Yaani la kumpwekesha Mwenyezi Mungu- "Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu", ikikumbusha kutakasa matendo kwaajili ya Mwenyezi Mungu katika ibada, hata kama makafiri wote watachukia. Kisha akataja Abdullahi bin Zubeir Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao kuwa -Mjumbe wa Mwenyezi Mungu- Rehema na Amani ziwe juu yake alikuwa anapotoa salamu katika swala yake, yanakuwa matamshi yake ni kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa namna hii, na alikuwa akinyanyua sauti yake kwa maneno haya kwaajili ya kumfundisha aliyehudhuria pamoja naye katika watu wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ni Sunna kudumu na nyiradi hizi zinazokusanya sifa kamilifu baada ya kila swala ya faradhi.
  2. Mzunguko wa dini nzima uko katika kutakasa nia kwaajili ya Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake; Haya mawili ndiyo yanayouendesha uislamu.
  3. Pupa ya maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- juu ya kutekeleza sunna na kuitangaza.
  4. Muislamu hujifaharisha kwa dini yake na anadhihirisha nembo zake pamoja na chuki za makafiri.
Ziada