عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«لَا تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ مَقَابِرَ، إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْفِرُ مِنَ الْبَيْتِ الَّذِي تُقْرَأُ فِيهِ سُورَةُ الْبَقَرَةِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 780]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Msiyafanye majumba yenu kuwa makaburi, hakika Shetani hukimbia kutoka katika nyumba inayosomwa suratul Baqara ndani yake".

[Sahihi] - [Imepokelewa Imamu Muslim] - [Swahiih Muslim - 780]

Ufafanuzi

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake.
Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
  2. Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
  3. Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (62)