عن أبي الدرداء رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ حَفِظَ عَشْرَ آيَاتٍ مِنْ أَوَّلِ سُورَةِ الكَهْفِ، عُصِمَ مِنَ الدَّجَّالِ». وفي رواية: «مِنْ آخِرِ سُورَةِ الكَهْف».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 809]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dardai radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakayehifadhi aya kumi za mwanzo wa suratul Kahf, atakingwa na Dajali". Na katika riwaya nyingine: "Za mwisho wa suratul Kahf".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 809]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayehifadhi aya kumi kwa moyo wake za mwanzo wa suratul Kahaf atakingwa na kuepushwa na kuhifadhiwa na fitina za Masihi Dajali atakayetoka zama za mwisho na atadai uungu, na fitina zake ni fitina kubwa itakayotokea katika Ardhi tangu kuumbwa kwa Adam mpaka kusimama kwa Kiyama; kwa yale aliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu katika mambo ya ajabu ambayo atawafitinisha kwayo watakaomfuata, na hii ni kwa sababu mwanzo wa suratul Kahaf kuna maajabu na miujiza mikubwa kuliko fitina na za Dajali kwa watu, atakayezizingatia hatofitinika na Dajali. Na katika riwaya nyingine: Ni aya kumi za mwisho wa sura kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Hivi wanadhani wale waliokufuru kuwa wanaweza kujifanyia..."