+ -

عن عثمان بن عفان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 245]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 245]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetawadha kwa kuchunga sunna za udhu na adabu zake, hilo litakuwa katika sababu za kusamehewa makosa na kufuta madhambi, "Mpaka yatoke" madhambi yake kutoka chini ya kucha za mikono yake na miguu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kutilia umuhimu wa kujifunza udhu na sunna zake na adabu zake, na kuzifanyia kazi.
  2. Ubora wa udhu, nakuwa hilo ni kafara ya madhambi madogo, ama makubwa ni lazima kufanya toba.
  3. Sharti za kutoka kwa madhambi ni kuukamilisha udhu na kuuleta bila mapungufu kama alivyobainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  4. Kufutwa kwa madhambi katika hadithi hii kumefungamanishwa na kuyaepuka madhambi makubwa na kuyaombea toba, amesema Mtukufu: "Ikiwa mtayaepuka madhambi makubwa mnayokatazwa tutakusameheni makosa yenu" [An-Nisaa: 31].