عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعاً: "إن من شرار الناس من تُدركهم الساعة وهم أحياء، والذين يتخذون القبور مساجد".
[حسن] - [رواه أحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillah bin Mas'udi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Hakika katika watu waovu ni wale kitakaowakuta kiyama wakiwa hai, na wale wanaoyafanya makaburi kuwa ni misikiti."
Ni nzuri - Imepokelewa na Ahmad

Ufafanuzi

Anaeleza rehema na Amani zimfikie kuhusu wale kitakaowakuta kiyama nao wakiwa hai kuwa wao ni katika watu waovu, na miongoni mwao ni wale wanaoswali katika makaburi na kuyaelekea na wanajenga juu yake vikuba (vibanda) na hii ni tahadhari kwa umma wake usijekufanya pamoja na makaburi ya Manabii wao na wema wao mfano wa kitendo cha watu hao waovu.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Kuthibitishwa kusimama kiyama.
  2. Kuwa kiyama kitasimama juu ya watu waovu.
  3. Uharamu wa kujenga misikiti juu ya makaburi au kuswalia hapo bila ya kujenga; kwasababu neno masjidi (msikiti), ni jina la mahala anaposujudia mtu, hata kama hakuna jengo.
  4. Tahadhari ya kutoswalia katika makaburi kwasababu ni njia inayopelekea katika ushirikina.
  5. Kuwa mwenye kuyafanya makaburi ya watu wema kuwa misikiti kwaajili ya swala huyo ni katika viumbe waovu zaidi, hata kama lengo lake ni kujiweka karibu na Mwenyezi Mungu.
  6. Tahadhari ya ushirikina na njia zake na yote yanayopelekea hilo, vyovyote litakavyokuwa lengo la njia hiyo.
  7. Muujiza wa Mtume rehema na Amani zimfikie- kiasi kwamba imetokea kama alivyoeleza, kama kufanywa misikiti juu ya makaburi.
Ziyada