عن أنس بن مالك رضي الله عنه أنَّ أَعْرَابِيًا قال لرسول الله صلى الله عليه وسلم: مَتَى السَّاعَة؟ قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَا أَعْدَدْتَ لَهَا؟» قال: حُبُّ الله ورَسُولِه، قال: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi bin Maliki- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba bedui alisema kumwambia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Ni lini kiyama? Akasema Mtume -Rehema na Aman ziwe juu yake: "Umekiandalia nini?" Akasema: Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Akasema: "Wewe pamoja na uliyempenda".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Aliuliza bedui (Ni lini kiyama?) Na laiti Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: angelijibu sijui, asingeikinaisha nafsi ya bedui, lakini hekima ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ikatoka katika upande wa chanzo cha swali na kuelekea katika kumjibu kwa yale yanampasa juu yake ukiachilia mbali yale asiyoyamiliki, nayo ni njia inayoitwa njia ya uamuzi, akasema Mtume- Rehema na Amani ziwe juu yake- "Umeandaa nini kwaajili yake?" Nalo ni swali la kuzindua, na kukumbusha yanayomlazimu kuyafikiria ndani yake, na kushughulika nayo, Bedui akasema: "Mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake", likaja jibu la bedui kwa uombaji wa msamaha unaopelekea mapenzi ya dhati, na imani, na kujivua kutegemea matendo yake pekee, na riwaya ya pili inathibitisha maana hii katika kauli ya bedui: "Sijaiandalia swaumu nyingi, wala swala nyingi, wala sadaka nyingi, lakini mimi ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake"; Na kwaajili hii likaja jibu la Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa "Wewe pamoja na yule uliyempenda". Basi katika hadithi hii tunahimizwa juu ya kuwapenda sana Mitume, na kuwafuata kulingana na ngazi zao, na tahadhari ya kuwapenda wasiyokuwa wao, kwasababu mapenzi ni dalili inayoonyesha mahusiano ya nguvu kati ya mpenzi kwa mpenzi wake, na kuendana na tabia zake, na kuiga kwake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno
Kuonyesha Tarjama