عن عَائِشَةَ رضيَ الله عنها قالت: إِنِّي سمعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«لَا صَلَاةَ بِحَضْرَةِ الطَّعَامِ، وَلَا هُوَ يُدَافِعُهُ الْأَخْبَثَانِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 560]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakuna swala chakula kinapokuwa tayari, na wala hakuna (swala) akiwa anazuia na kubana vichafu viwili(Haja kubwa na ndogo)".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 560]
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuswali kinapotengwa chakula kile anachokitamani mwenye kuswali, na moyo wake umefungamana nacho.
Na vile vile amekataza kuswali mtu akiwa anazuia haja mbili -nazo ni mkojo na haja kubwa-, kwakuwa atashughulika na kuzuia udhia.