+ -

عَن أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ فِي صَلاَتِهِمْ»، فَاشْتَدَّ قَوْلُهُ فِي ذَلِكَ، حَتَّى قَالَ: «لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 750]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Hivi wana nini watu! wananyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala zao", ikazidi ukali kauli yake katika hilo, mpaka akasema: "Hakika, ni ima waache kufanya hivyo, au yatapofuliwa macho yao".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 750]

Ufafanuzi

Aliwatahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wale wanaonyanyua macho yao mbinguni ndani ya swala wakati wa dua au kinginecho, kisha karipio lake likawa kali na akatangaza adhabu rehema na amani ziwe juu yake kwa wanaofanya hivyo kwamba yanahofiwa macho yao kupofuliwa na yakanyakuliwa kwa haraka kwa namna wasiyoitarajia, wakajikuta tayari wamepoteza neema ya macho.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kubainisha kwake haki; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake hakumtaja mkosefu; kwa sababu lengo ni kubainisha haki na tayari imekwisha tendeka; na kwa sababu ndani yake kuna kumsitiri mkosefu na inahamasisha zaidi mtu kukubali ukweli.
  2. Katazo la msisitizo, na ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua macho yake juu mbinguni ndani ya swala.
  3. Amesema katika kitabu cha Aunul Ma'buud: Na sababu katika hilo ni kwamba atakaponyanyua macho yake juu mbinguni atakuwa katoka katika nembo ya kibla na ameipuuza na katoka katika muonekano wa swala pia.
  4. Kunyanyua macho kunaondoa utulivu ndani ya swala.
  5. Ukubwa wa hadhi ya swala, na kwamba ni wajibu kwa wenye kusali wawe katika adabu kamili pamoja na Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama