عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ نَسِيَ صَلَاةً فَلْيُصَلِّ إِذَا ذَكَرَهَا، لَا كَفَّارَةَ لَهَا إِلَّا ذَلِكَ: {وَأَقِمِ الصَّلاةَ لِذِكْرِي} [طه: 14]».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 597]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo: "Na simamisha swala kwa ajili ya kunitaja mimi" [Twaha: 14].
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 597]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesahau kutekeleza swala ya faradhi mpaka ukatoka wakati wakati wake, basi anatakiwa aende mbio na afanye haraka kuilipa pale anapoikumbuka, amesema Allah katika kitabu chake kitukufu: "Na usimamishe swala kwa ajili ya kunitaja" [Twaha: 14] Simamisha swala zilizosahaulika unapozikumbuka.