عن بريدة بن الحصيب رضي الله عنه أنه قال:
بَكِّرُوا بِصَلَاةِ الْعَصْرِ، فَإِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ تَرَكَ صَلَاةَ الْعَصْرِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 553]
المزيــد ...
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa amesema:
Iswalini mapema swala ya Lasiri, kwani Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 553]
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuchelewesha swala ya Lasiri nje ya wakati wake kwa makusudi, nakuwa mwenye kufanya hivyo yatakuwa yamebatilika matendo yake na yameharibika matendo yake na yameenda patupu.