+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها:
أَنَّ أُمَّ سَلَمَةَ ذَكَرَتْ لِرَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَنِيسَةً رَأَتْهَا بِأَرْضِ الْحَبَشَةِ، يُقَالُ لَهَا مَارِيَةُ، فَذَكَرَتْ لَهُ مَا رَأَتْ فِيهَا مِنَ الصُّوَرِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أُولَئِكَ قَوْمٌ إِذَا مَاتَ فِيهِمُ الْعَبْدُ الصَّالِحُ، أَوِ الرَّجُلُ الصَّالِحُ، بَنَوْا عَلَى قَبْرِهِ مَسْجِدًا، وَصَوَّرُوا فِيهِ تِلْكَ الصُّوَرَ، أُولَئِكَ شِرَارُ الْخَلْقِ عِنْدَ اللهِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 434]
المزيــد ...

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:
Yakwamba Mama Salama alimsimulia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kisa cha kanisa aliloliona katika ardhi ya Ethiopia, likiitwa kanisa la Mtakatifu Maria, akasimulia aliyoyaona ndani yake miongoni mwa picha, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Watu hao anapokufa kwao mja mwema, au mwanaume mwema, wanajenga juu ya kaburi lake mahala pakuabudia, na wanachora ndani yake picha hizo, hao ndio viumbe waovu zaidi mbele ya Allah

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 434]

Ufafanuzi

Amesimulia mama wa waumini mama Salama radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba alipokuwa katika ardhi ya Ethiopia aliona Kanisa -linaloitwa kwa jina la Mtakatifu Maria- ndani yake kukiwa na picha na mapambo na michoro; akastaajabu kwa kitendo hicho!. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akafafanua sababu za kuwekwa picha hizo; Akasema: Hakika hao unaowataja hapa walikuwa anapokufa kwao mtu mwema wanajenga Msikiti juu ya kaburi lake, na wanasali ndani yake, na wanachoro picha hizo, Na akabainisha kuwa mfanyaji wa hilo ni kiumbe muovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu kitendo chake hicho kinapelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kujenga Misikiti juu ya makaburi, au kuswali hapo, au kuzika maiti ndani ya msikiti; hii ikiwa ni kuziba njia za kuelekea katika ushirikina.
  2. Kujenga Misikiti juu ya makaburi, na kutundika picha, hiki ni kitendo cha Mayahudi, nakuwa mwenye kufanya hivi atakuwa kafanana nao.
  3. Uharamu wa kutengeneza picha za viumbe hai (wenye roho).
  4. Atakayejenga msikiti juu ya kaburi na akachoro ndani yake picha, huyu ni katika viumbe waovu zaidi kuliko wote mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Sheria imeuhami sana upande wa tauhidi kwa himaya iliyokamilika, kwa kuziba njia zote ambazo zinaweza kusababisha kufika katika ushirikina.
  6. Katazo la kuchupa mipaka kwa watu wema; kwani ni sababu ya kuingia katika shirki.
Ziada