+ -

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَتَبَاهَى النَّاسُ فِي الْمَسَاجِدِ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي وابن ماجه] - [سنن أبي داود: 449]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -radhi za Allah ziwe juu yake- Ya kwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakitosimama Kiyama mpaka watu wajifaharishe katika Misikiti".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 449]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa miongoni mwa dalili za kukaribia kwa Kiyama na kumalizika kwa Dunia, ni watu kujifaharisha kwa kuipamba Misikiti yao, au kujifaharisha kwa dunia yao ndani ya misikiti ambayo haikujengwa ila kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kujifaharisha kwa Misikiti, na kwamba ni jambo lisilokubalika; kwa sababu kitendo hicho hakikufanyika kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  2. Katazo la kuipamba Misikiti kwa rangi na vito na nakshi, na maandishi; kwa sababu ndani yake kuna kuwashughulisha wenye kuswali wanapoyatazama.
  3. Amesema Assanadi: Hadithi ni miongoni mwa zile ambazo uhalisia unashuhudia yaliyosemwa, ni miongoni mwa miujiza ya kushangaza ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama