عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«صَلَاةٌ فِي مَسْجِدِي هَذَا خَيْرٌ مِنْ أَلْفِ صَلَاةٍ فِيمَا سِوَاهُ إِلَّا الْمَسْجِدَ الْحَرَامَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1190]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Kusali ndani ya Msikiti wangu huu ni bora kuliko sala elfu moja zinazo swaliwa nje ya Msikiti huu isipokuwa Msikiti wa Makka".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1190]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ubora wa kuswalia katika msikiti wake, nakuwa ni thawabu bora kuliko swala elfu moja (1000) katika misikiti mingine katika misiti ya ardhini, isipokuwa msikiti mtukufu wa Makka, huo ni bora kuliko swala ya msikiti wake rehema na amani ziwe juu yake.