عَنْ أَبِي قَتَادَةَ السَّلَمِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ أَنْ يَجْلِسَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 444]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Qatada As-sulami Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi asali rakaa mbili kabla hajakaa".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 444]
Amemhimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mwenye kuja msikitini na akaingia katika wakati wowote, na kwa lengo lolote, asali rakaa mbili kabla hajakaa, nazo ni rakaa mbili za salamu ya msikiti.