+ -

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ:
حَفِظْتُ مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَشْرَ رَكَعَاتٍ: رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ المَغْرِبِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ العِشَاءِ فِي بَيْتِهِ، وَرَكْعَتَيْنِ قَبْلَ صَلاَةِ الصُّبْحِ، وَكَانَتْ سَاعَةً لاَ يُدْخَلُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيهَا، حَدَّثَتْنِي حَفْصَةُ أَنَّهُ كَانَ إِذَا أَذَّنَ المُؤَذِّنُ وَطَلَعَ الفَجْرُ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ، وَفِي لَفْظٍ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُصَلِّي بَعْدَ الْجُمُعَةِ رَكْعَتَيْنِ.

[صحيح] - [متفق عليه بجميع رواياته] - [صحيح البخاري: 1180]
المزيــد ...

Imeokewa Kutoka kwa bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema :
Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi: Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, na rakaa mbili kabla ya swala ya Alfajiri, na muda huo ulikuwa ni wakati ambao haruhusiwi yeyote kuingia kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, Hafswa ndiye aliyenisimulia kuwa alikuwa anapoadhini muadhini na ikachomoza Alfajiri anaswali rakaa mbili, na katika riwaya nyingine: Nikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akiswali baada ya Ijumaa rakaa mbili.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim katika riwaya zake zote] - [صحيح البخاري - 1180]

Ufafanuzi

Anabainisha Abdullahi bin Omari Radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake: Yakuwa miongoni mwa swala za sunna alizozihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni rakaa kumi na huitwa kuwa ni sunna zilizopangiliwa, Rakaa mbili kabla ya Dhuhuri, na rakaa mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi nyumbani kwake, na rakaa mbili baada ya Ishaa nyumbani kwake, Na kabla ya Alfajiri rakaa mbili, Zikatimia rakaa kumi. Na ama swala ya Ijumaa aliswali baada yake rakaa mbili.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Imendezeshwa kuswali rakaa hizi zilizopangiliwa, na kudumu nazo.
  2. Sheria ya kuswali sunna nyumbani.