عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الْأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْئًا، وَمَنْ دَعَا إِلَى ضَلَالَةٍ كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الْإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ، لَا يَنْقُصُ ذَلِكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئًا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2674]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayelingania katika uongofu, atakuwa kwake kapata malipo mfano wa malipo ya aliyemfuata, halipunguzi hilo chochote katika malipo yao, na atakayelingania katika upotofu atakuwa kwake na madhambi mfano wa madhambi ya yule aliyemfuata, halipunguzi hilo katika madhambi yao chochote".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2674]
Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayewaelekeza na kuwajulisha na kuwahamasisha watu katika njia ya haki na kheri kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na malipo mfano wa malipo atakayoyapata aliyemfuata katika hilo, na hilo halitopunguza katika malipo ya mfanyaji chochote. Na atakaye waelekeza watu na kuwaonyesha njia ya batili na shari ambayo ina dhambi ndani yake na makosa au jambo lisilo la halali, kwa kauli au kitendo, basi atakuwa na madhambi mfano wa madhambi ya yule atakayemfuata, pasina ya kupunguza hilo katika madhambi yao chochote.