عن سلمة بن الأكوع رضي الله عنه : أن رجلا أكَلَ عند رسول الله صلى الله عليه وسلم بشماله، فقال: «كُلْ بيمينك» قال: لا أستطيع. قال: «لا استطَعْتَ» ما مَنَعَهُ إلا الكِبْر فما رَفَعَهَا إلى فِيهِ.
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Salama bin Akwa'i -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba mtu mmoja alikula kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "kula kwa mkono wako wa kulia", akasema: siwezi. akasema: "Hutoweza", hakuna kilichomzuia isipokuwa ni kiburi, basi hakuweza tena kuunyanyua kufika kinywani kwake.
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Alikula mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa mkono wa kushoto kwa kiburi; akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kumwambia "Kula kwa mkono wako wa kulia" akasema kwa ukaidi: Siwezi!. hali yakuwa si mkweli katika hilo; akamuombea dua mbaya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kusema: "Hutoweza". Hakuweza tena kunyanyua mkono wake kufika kinywani kwake, na hili ni kwasababu alipooza kwasababu ya dua mbaya ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwake; kwa kiburi chake na kukataa kwake amri ya kiutume.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama