عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ عَادَ مَرِيضًا، لَمْ يَحْضُرْ أَجَلُهُ فَقَالَ عِنْدَهُ سَبْعَ مِرَارٍ: أَسْأَلُ اللَّهَ الْعَظِيمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ أَنْ يَشْفِيَكَ، إِلَّا عَافَاهُ اللَّهُ مِنْ ذَلِكَ الْمَرَضِ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وأحمد] - [سنن أبي داود: 3106]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema:
"Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 3106]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hakuna muislamu atakayemtembelea muislamu katika maradhi yake, ambaye muda wa mauti yake haujafika, kisha aliyekwenda kumtembelea akamuombea mgonjwa kwa kusema: "Namuomba Allah Mtukufu" katika dhati yake na sifa zake na vitendo vyake, "Mola wa Arshi Tukufu akuponye", na akarudia mbele yake mara saba, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kutokana na maradhi hayo.