+ -

عَنْ عُثْمَانَ بْنِ أَبِي الْعَاصِ الثَّقَفِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ شَكَا إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَجَعًا يَجِدُهُ فِي جَسَدِهِ مُنْذُ أَسْلَمَ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«ضَعْ يَدَكَ عَلَى الَّذِي تَأَلَّمَ مِنْ جَسَدِكَ، وَقُلْ بِاسْمِ اللهِ ثَلَاثًا، وَقُلْ سَبْعَ مَرَّاتٍ أَعُوذُ بِاللهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2202]
المزيــد ...

Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi Ath-thaqafi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maumivu anayoyapata katika mwili wake tangu aliposilimu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia:
"Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2202]

Ufafanuzi

Othman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya mtu kujifanyia kisomo cha ruqya yeye mwenyewe kama ilivyokuja katika hadithi.
  2. Malalamiko -pasina kuchukizwa na hali wala kupingana na Kadari- hakupingani na kutawakali na subira.
  3. Dua ni miongoni mwa kuchukua sababu, na ndio maana ni lazima kushikamana na matamshi yake na idadi yake.
  4. Dua hii inasomwa kwa maumivu ya kila kiungo.
  5. Kuweka mkono juu ya mahala palipo na maumivu wakati wa kusoma dua hii.