عن عقبة بن عامر رضي الله عنه مرفوعاً: «إن أحَقَّ الشُّروط أن تُوفُوا به: ما استحللتم به الفروج».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Uqbah bin Aamir -Radhi za Allah ziwe juu yake- akisimulia kutoka kwa Mtume: " Hakika masharti yenye haki zaidi ya nyinyi kuyatekeleza ni yale mliyohalalisha kwayo nyuchi".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Kila mmoja katika wanandoa ana makusudio na malengo ya kudumu katika mkataba wa ndoa, hivyo akaweka sharti kwa mwenzie ili ashikamane nazo na akataka zitekelezwe, na zinaitwa kuwa ni sharti katika ndoa, nazo ni zile zinazozidi katika sharti za ndoa ambazo ndoa haikubaliki ispokuwa kwa sharti hizo. Na umekuja msisitizo juu ya kuzitekeleza; kwasababu sharti katika ndoa zina heshima kubwa na kuzitimiza na kuzizingatia ni lazima; kwa kuwa kwake zimestahiki kuhalalisha na kustarehe na tupu.