عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ رَضيَ اللهُ عنهُما:
أَنَّ أُمَّهُ بِنْتَ رَوَاحَةَ سَأَلَتْ أَبَاهُ بَعْضَ الْمَوْهِبَةِ مِنْ مَالِهِ لِابْنِهَا، فَالْتَوَى بِهَا سَنَةً ثُمَّ بَدَا لَهُ، فَقَالَتْ: لَا أَرْضَى حَتَّى تُشْهِدَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى مَا وَهَبْتَ لِابْنِي، فَأَخَذَ أَبِي بِيَدِي وَأَنَا يَوْمَئِذٍ غُلَامٌ، فَأَتَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ أُمَّ هَذَا بِنْتَ رَوَاحَةَ أَعْجَبَهَا أَنْ أُشْهِدَكَ عَلَى الَّذِي وَهَبْتُ لِابْنِهَا، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا بَشِيرُ، أَلَكَ وَلَدٌ سِوَى هَذَا؟» قَالَ: نَعَمْ، فَقَالَ: «أَكُلَّهُمْ وَهَبْتَ لَهُ مِثْلَ هَذَا؟» قَالَ: لَا، قَالَ: «فَلَا تُشْهِدْنِي إِذن، فَإِنِّي لَا أَشْهَدُ عَلَى جَوْرٍ»، ولِمُسْلِمٍ: «فَأَشْهِدْ عَلَى هَذَا غَيْرِي».
[صحيح] - [متفق عليه، وله ألفاظ عديدة] - [صحيح مسلم: 1623]
المزيــد ...
Kutoka kwa Nuuman bin Bashiri radhi za Allah ziwe kwao yeye na baba yake:
Ya kwamba mama yake bint Rawaha alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake anazompa mwanaye, akasitisha kutoa kwa mwaka mzima, kisha akaona amjibu, akasema (Mama Nuuman): Siwezi kuridhika mpaka umfanye Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa shahidi kwa hivyo ulivyomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akamuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa mtoto huyu, binti Rawaha kapenda nikufanye wewe kuwa shahidi kwa zawadi nilizomzawadia mwanaye, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Bashiri una mtoto zaidi ya huyu?" Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wanao wote umewazadia kama huyu?" Akasema: Hapana. Akasema: "Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani siwezi kushuhudia dhulma", na kwa Imamu Muslim: "Kamtake ashuhudie mtu mwingine asiyekuwa mimi".
[Sahihi] - - [صحيح مسلم - 1623]
Ameeleza Nuuma bin Bashiri radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, ya kwamba mama yake Amra binti Rawaha radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza baba yake baadhi ya zawadi katika mali yake kwa mwanaye, akawa mzito, na akachelewa kumjibu kwa muda wa mwaka mzima, kisha akaona amjibu swali lake, akamhofia mwanaye Nuuman, akasema: Siridhii mpaka umfanye kuwa shahidi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kile ulichomzawadia mwanangu, baba yangu akanishika mkono na mimi wakati huo nikiwa kijana mdogo, akumuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mama wa kijana huyu, binti Rawaha kapendezwa nikufanye kuwa shahidi kwa kile nilichomzawadia mwanaye, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ewe Bashiri, je, una mtoto mwingine asiyekuwa huyu? Akasema: Ndiyo. Akasema: Je, wote umewazawadia mfano wa huyu. Akasema: Hapana. Akasema: Basi usinifanye mimi kuwa shahidi, kwani mimi sishuhudii upendeleo na dhulma. Na kwa Muslim alisema kwa kumkemea: Lakini mshuhudishe katika dhulma hii mwingine asiyekuwa mimi.