عن ابن عمر رضي الله عنهما:
أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى عَنِ الْقَزَعِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5921]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amekataza kunyoa kiduku.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5921]
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kunyoa baadhi ya nywele za kichwa na kuacha baadhi.
Na katazo linawahusu watu wote, mwanaume mtoto mdogo na mkubwa pia, ama mwanamke hatakiwi kunyoa nywele za kichwa chake.