+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال:
لعن رسول الله صلى الله عليه وسلم الرجل يلبس لِبْسَةَ المرأة، والمرأة تلبس لِبْسَةَ الرجل.

[صحيح] - [رواه النسائي في الكبرى وابن ماجه بمعناه وأحمد] - [السنن الكبرى للنسائي: 9209]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Amemlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume anayevaa vazi la mwanamke, na mwanamke anayevaa vazi la mwanaume.

[Sahihi] - - [السنن الكبرى للنسائي - 9209]

Ufafanuzi

Aliomba Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema za Mwenyezi Mungu kwa kila mwanaume atakayejifananisha na mwanamke katika mavazi maalumu kwa ajili ya wanawake; sawa sawa iwe katika muonekano au rangi au jinsi au namna ya uvaaji na kujipamba. Au kwa mwanamke kujifananisha na mavazi maalumu kwa wanaume vile vile, nalo ni dhambi katika madhambi makubwa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema Shaukani: Kumeharamishwa wanawake kujifananisha na wanaume na wanaume kujifananisha na wanawake; kwa sababu laana huwa haiwi ila kwa kufanya jambo lililoharamishwa.
  2. Amesema bin Uthaimiin: Zile wanazoshirikiana kati yao, mfano kama jezi au shati ambazo wanazivaa wanaume na wanawake hizi hazina tatizo, yaani hakuna tatizo akizivaa mwanaume na mwanamke; kwa sababu wanashirikiana.