عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال:
لعن النبي صلى الله عليه وسلم الوَاصِلَةَ والمُسْتَوْصِلَةَ، والوَاشِمَةَ والمُسْتَوشِمَةَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5947]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema:
Kamlaani Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa, na mwenye kuchora chata na mwenye kuchorwa.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5947]
Dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kulaaniwa na kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa makundi ya aina nne: La kwanza: Mwanamke mwenye kuunga nywele zake au za mwenzake kwa nywele zingine. La pili: Na mwenye kutaka kuungwa nywele, kwa kumuomba mwenzake amuunganishe nywele zake kwa nywele zingine. La tatu: Mwenye kupiga chata, na anayejichoma sindano katika sehemu ya mwili wake, kama uso au kiganja au kifua, na kuweka wanja au mfano wake, ili kubakie alama ya bluu, au kijani; kwa kutaka kujipamba au uzuri. La nne: Mwenye kutaka kupigwa chata, ni yule anayeomba kupigwa chata. Na matendo haya ni katika madhambi makubwa.