عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَا أَسْفَلَ مِنَ الكَعْبَيْنِ مِنَ الإِزَارِ فَفِي النَّارِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5787]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kilichoshuka chini ya kongo mbili katika kikoi hicho ni motoni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 5787]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushusha chini zaidi ya miguu kila kinachositiri kuanzia chini ya mwili wake kama nguo au suruali au kinginecho, na kinachokuwa zaidi ya kongo mbili katika miguu miongoni mwa kikoi kinachoburuza basi hicho ni motoni ikiwa ni adhabu kwake kwa kitendo hicho.