عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ:
رَجَعْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ مَكَّةَ إِلَى الْمَدِينَةِ حَتَّى إِذَا كُنَّا بِمَاءٍ بِالطَّرِيقِ تَعَجَّلَ قَوْمٌ عِنْدَ الْعَصْرِ، فَتَوَضَّؤُوا وَهُمْ عِجَالٌ، فَانْتَهَيْنَا إِلَيْهِمْ وَأَعْقَابُهُمْ تَلُوحُ لَمْ يَمَسَّهَا الْمَاءُ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَيْلٌ لِلْأَعْقَابِ مِنَ النَّارِ أَسْبِغُوا الْوُضُوءَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 241]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema:
Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 241]
Alisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kutia udhu kwa ajili ya swala ya Alaasiri baadhi ya Masahaba, mpaka ukaonekana weupe mwisho wa miguu yao kwa mtu mwenye kuitazama kwa kukosa maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni adhabu na maangamivu katika moto kwa wenye kufanya uzembe wa kuosha mwisho wa nyayo wakati wa udhu, na akawaamrisha wapitilize katika kuukamilisha udhu.