عَنْ أَبِي ثَعْلَبَةَ الخُشَنِيِّ جُرْثُومِ بن نَاشِرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَال:
«إِنَّ اللَّهَ فَرَضَ فَرَائِضَ فَلَا تُضَيِّعُوهَا، وَحَدَّ حُدُودًا فَلَا تَعْتَدُوهَا، وَحَرَّمَ أَشْيَاءَ فَلَا تَنْتَهِكُوهَا، وَسَكَتَ عَنْ أَشْيَاءَ رَحْمَةً لَكُمْ غَيْرَ نِسْيَانٍ فَلَا تَبْحَثُوا عَنْهَا».
[قال النووي: حديث حسن] - [رواه الدارقطني في سننه، وغيره] - [الأربعون النووية: 30]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Tha'laba Al-Khushani Jurthuum bin Naashiri radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu amefaradhisha faradhi basi msizipoteze, na akaweka mipaka basi msiivuke, na akaharamisha vitu basi msivivamie, na akayanyamazia mambo kwa kukuhurumieni si kwa kusahau basi msiyatafute".
[قال النووي: حديث حسن] - [رواه الدارقطني في سننه وغيره] - [الأربعون النووية - 30]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.