عَن عَلِيٍّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
أَخَذَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَرِيرًا بِشِمَالِهِ، وَذَهَبًا بِيَمِينِهِ، ثُمَّ رَفَعَ بِهِمَا يَدَيْهِ، فَقَالَ: «إِنَّ هَذَيْنِ حَرَامٌ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي، حِلٌّ لِإِنَاثِهِمْ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي وابن ماجه] - [سنن ابن ماجه: 3595]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ally bin Abii Twaalib radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake Hariri kwa mkono wake wa kushoto, na dhahabu kwa mkono wake wa kulia, kisha akazinyanyua kwa mikono yake, akasema: "Hakika vitu hivi viwili ni haramu kwa wanaume wa umma wangu, ni halali kwa wanawake wao".
[Sahihi] - - [سنن ابن ماجه - 3595]
Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake nguo ya hariri au kipande chake, kwa mkono wake wa kushoto, na akachukua pambo la dhahabu au mfano wake kwa mkono wake wa kulia, kisha akasema: Hakika hariri na dhahabu ni haramu kuvivaa kwa wanaume, ama wanawake hivyo ni halali kwao.