عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الذَّهَبُ بِالذَّهَبِ، وَالْفِضَّةُ بِالْفِضَّةِ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ، وَالْمِلْحُ بِالْمِلْحِ، مِثْلًا بِمِثْلٍ، سَوَاءً بِسَوَاءٍ، يَدًا بِيَدٍ، فَإِذَا اخْتَلَفَتْ هَذِهِ الْأَصْنَافُ، فَبِيعُوا كَيْفَ شِئْتُمْ، إِذَا كَانَ يَدًا بِيَدٍ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1587]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ubada bin Swaamit -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
"Uuzaji unakuwa ni kuuza Dhahabu kwa dhahabu, na fedha kwa fedha, ngano kwa ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano kwa ngano (iliokobolewa), na tende kwa tende, na chumvi kwa chumvi, mfano kwa mfano, sawa kwa sawa, mkono kwa mkono, zikitofautiana aina hizi, basi uzeni mtakavyo, ikiwa mkono kwa mkono".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1587]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake namna ya biashara sahihi katika aina sita za riba, nazo ni: Dhahabu, fedha, ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano (iliyokobolewa), na tende, na chumvi, ikiwa ni katika aina hiyo hiyo, kama kuuza dhahabu kwa dhahabu na fedha kwa fedha....ni lazima kuwe na sharti mbili: Ya kwanza: Kufanana katika uzito ikiwa ni kitu kinachopimika kama dhahabu na fedha, au kufanana katika kipimo ikiwa ni kitu kinachopimika, kama ngano (ambayo haijakobolewa) na ngano (iliyokobolewa) na tende na chumvi. Ya pili: Ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa, na hilo lifanyike katika kikao cha makubaliano ya biashara. Zikitofautiana aina zote hizi kama kuuza dhahabu kwa fedha, na tende kwa ngano kwa mfano, itafaa kuuza kwa sharti moja, nayo ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa katika kikao cha makubaliano, isipofanyika hivyo biashara itakuwa batili, na muuzaji na mnunuzi watakuwa wameingia ndani ya riba katika hilo wote wawili.