عَنْ مَالِكِ بْنِ أَوْسِ بْنِ الْحَدَثَانِ أَنَّهُ قَالَ: أَقْبَلْتُ أَقُولُ مَنْ يَصْطَرِفُ الدَّرَاهِمَ؟ فَقَالَ طَلْحَةُ بْنُ عُبَيْدِ اللهِ وَهُوَ عِنْدَ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رضي الله عنهما: أَرِنَا ذَهَبَكَ، ثُمَّ ائْتِنَا، إِذَا جَاءَ خَادِمُنَا، نُعْطِكَ وَرِقَكَ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: كَلَّا، وَاللهِ لَتُعْطِيَنَّهُ وَرِقَهُ، أَوْ لَتَرُدَّنَّ إِلَيْهِ ذَهَبَهُ، فَإِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«الْوَرِقُ بِالذَّهَبِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالْبُرُّ بِالْبُرِّ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالشَّعِيرُ بِالشَّعِيرِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ، وَالتَّمْرُ بِالتَّمْرِ رِبًا، إِلَّا هَاءَ وَهَاءَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1586]
المزيــد ...
Kutoka kwa Maliki bin Ausi bin Hadathani yakuwa yeye alisema: Niligeuka nikasema ni nani anayechenji pesa? Twalha bin Ubaidillah akasema wakati akiwa kwa Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yao wote: Tuonyeshe Dhahabu yako, kisha tuletee, atakapokuja mfanyakazi wetu tutakupa pesa yako, akasema Omari bin Khattwab: Hapana, ni lazima utampa haki yake, au umrejeshee Dhahabu yake, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Fedha kwa dhahabu ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na ngano isiyokobolewa ni riba, ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na shairi (ngano iliyokobolewa ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono, na tende kwa tende ni riba ila kama itakuwa mkono kwa mkono".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1586]
Taabii (Mwanafunzi wa Maswahaba) Malik bin Ausi anaeleza kuwa alikuwa na dinari za dhahabu, na alitaka kuzibadilisha kwa dirham za fedha, basi Twalha bin Ubaidillah (radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia: Tupe dinari zako nizione! Kisha akamwambia baada ya kuamua kununua: Njoo kwetu ikiwa mtumwa wetu atakuja baadaye tutakupe dirham za fedha, Omari bin Khattab Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alilaani aina hii ya muamala (biashara), na akaapa kwa Twalha kuwa atalipa fedha sasa, au amrudishie dhahabu yake aliyoichukua yeye, akasema kuwa kuuza fedha kwa dhahabu, au kinyume chake, lazima kupokea kuwe mkono kwa mkono, vinginevyo biashara hiyo itakuwa ni riba iliyoharamishwa na uuzaji batili, Dhahabu haiuzwi kwa fedha, wala fedha kwa dhahabu, isipokuwa mkono kwa mkono, na kufanyike kubadilishana, wala haiuzwi kwa ngano, na shayiri kwa shayiri, na tende kwa mfano wake, kipimo kwa kipimo, mkono kwa mkono; na haijuzu kuachana katika makubaliano kabla ya kuimiliki.