+ -

عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«تَعَاهَدُوا هَذَا الْقُرْآنَ، فَوَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لَهُوَ أَشَدُّ تَفَلُّتًا مِنَ الْإِبِلِ فِي عُقُلِهَا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 791]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Mussa Al-Ash'ary-Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Shikamaneni vizuri na hii Qur'ani, namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammadi iko mkononi mwake, hutoroka kwa kasi mno kuliko hata Ngamia katika kamba yake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 791]

Ufafanuzi

Ameamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kushikamana na Qur'ani na kudumu na kuisoma ili mtu asiisahau baada yakuwa kaihifadhi katika kifua chake, na akalisisitiza hilo kwa kiapo chake -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Qur'ani hujitoa haraka mno na kuondoka kutoka vifuani kuliko hata Ngamia aliyefungwa, naye ni yule aliyekazwa kwa kamba kati kati ya muhundi, mtu akikaa karibu naye atamshika, na akimuacha ataondoka na atapotea.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Aliyehifadhi Qur'ani akidumu katika kuisoma kila mara itabakia kuwa imehifadhiwa katika moyo wake, na asipofanya hivyo itaondoka na ataisahau.
  2. Katika faida za kushikana na Qur'ani ni: Malipo na thawabu, na kunyanyuliwa daraja siku ya Kiyama.