عَن أَبي مُوْسى الأَشْعريِّ رضي الله عنه قال: قال رسولُ اللهِ صلى اللهُ عليه وسلم:
«مَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْأُتْرُجَّةِ، رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا طَيِّبٌ، وَمَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ التَّمْرَةِ، لَا رِيحَ لَهَا وَطَعْمُهَا حُلْوٌ، وَمَثَلُ الْمُنَافِقِ الَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ مَثَلُ الرَّيْحَانَةِ، رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ، وَمَثَلُ الْمُنَافِقِ الَّذِي لَا يَقْرَأُ الْقُرْآنَ كَمَثَلِ الْحَنْظَلَةِ، لَيْسَ لَهَا رِيحٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ».

[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ariy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu, na mfano wa mnafiki mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa Ua la Raihana harufu yake nzuri lakini ladha yake chungu, na mfano wa mnafiki ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tango pori, halina harufu na ladha yake chungu".

Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake migawanyiko ya watu katika kuisoma Qur'ani na kunufaika nayo.
Sehemu ya kwanza: Ni muumini anayesoma Qur'ani na ananufaika nayo, yeye ni mfano wa chenza, lina ladha nzuri na harufu nzuri na rangi nzuri, na manufaa yake ni mengi, kwani yeye huyafanyia kazi anayoyasoma, na kuwanufaisha waja wa Mwenyezi Mungu.
Sehemu ya pili: Ni muumini asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tende, ladha yake tamu, lakini haina harufu, moyo wake umejawa na imani mfano wa tende ilivyojawa utamu katika ladha yake na juu yake, na kutosikika harufu yake ambayo watu huinusa; kwa kutosikika kisomo toka kwake ambacho watu watapata raha kwa kukisikiliza
Sehemu ya tatu: Mnafiki anayesoma Qur'ani, yeye ni mfano wa Ua Raihana, lina harufu nzuri na ladha yake chungu, kwakuwa hakuurekebisha moyo wake kwa imani, na hakuifanyia kazi Qur'ani, na anaonekana mbele za watu kuwa ni muumini, harufu yake nzuri inafanana na kisomo chake, na ladha ya chungu inafanana na ukafiri wake.
Sehemu ya nne: Mnafiki asiyeisoma Qur'ani, yeye ni mfano wa tango pori, kiasi kwamba halina harufu nzuri, na ladha yake ni chungu, kukosekana kwa harufu yake kumefanana na harufu yake; kwa kutoisoma, na uchungu wa ladha yake unafanana na uchungu wa ukafiri wake, ndani mwake kuko tupu hakuna imani, na nje yake hakuna manufaa, bali kuna madhara.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa ubora wa mwenye kuibeba Qur'ani mwenye kuifanyia kazi.
  2. Miongoni mwa njia za ufundishaji ni kupiga mifano; ili kusogeza karibu uelewa.
  3. Inatakiwa muislamu awe na kiwango maalum cha fungu katika kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu.