عن عثمان رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 5027]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Mmbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [Swahiih Al Bukhaariy - 5027]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu bora na aliye na daraja ya juu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu: Ni yule aliyejifunza Qur'ani, kwa kuisoma na kuihifadhi na kuisoma vizuri na kuielewa na kuitafsiri, na akamfundisha mwingine kile alichonacho katika elimu za Qur'ani pamoja na kuifanyia kazi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa utukufu wa Qur'ani, nakuwa ndio maneno bora; kwani ni maneno ya Allah.
  2. Mwanafunzi bora ni yule anayefundisha wengine, hatosheki kujifunza mwenyewe pekee.
  3. Kujifunza Qur'ani na kuifundisha kunakusanya, kuisoma na maana yake na hukumu zake.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (63)