عَنْ عَلِيٍّ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«قُلِ اللهُمَّ اهْدِنِي وَسَدِّدْنِي، وَاذْكُرْ بِالْهُدَى هِدَايَتَكَ الطَّرِيقَ، وَالسَّدَادِ سَدَادَ السَّهْمِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2725]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -rehema na amani ziwe juu yake:
"Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2725]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuamrisha Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake amtake Mwenyezi Mungu na amuombe na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu niongoze" na unielekeze na unijulishe "na unisimamie" na uniafikishe, na unifanye kuwa na msimamo katika mambo yangu yote.
Uongofu: Ni kuijua haki kwa ujumla na kwa ufafanuzi, na kuwezeshwa kuifuata kwa wazi na kwa siri.
Na kusimamiwa: Ni kuwezeshwa na kuwa na msimamo katika mambo yote katika yale ya kweli juu ya haki, nayo ni njia iliyonyooka katika kauli na vitendo na itikadi.
Na hii ni kwa sababu jambo lisiloonekana hueleweka wazi kupitia jambo linaloonekana; Hivyo kumbuka unapokuwa unaomba dua hii kuwa: "Uongofu: Ni kuongozwa njia" Hivyo, hudhurisha moyo wako nawe ukiwa unaomba uongofu mfano wa uongofu wa aliyesafarini, kwani huwa hatoki nje ya njia si kulia wala kushoto; na hii ni ili asalimike na kupotea, na kwa hilo anapata usalama, na atafika haraka katika lengo lake.
"Na kuafikishwa nakupatia: Ni kupatia kwa mshale" Wewe chunguza wakati wa kulenga kwako mshale katika uharaka wa kufika kwake na kukipata ulichokusudia kukipiga, mrusha mishale anaporusha katika lengo basi huhakikisha ameulenga vizuri mshale katika kile alichokikusudia, hivyo hivyo na wewe unamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa yote unayoyakusudia basi yawe katika mfano wa mshale; utakuwa katika kuomba kwako umeomba kiwango cha juu zaidi cha uongofu, na mwisho wa kusimamiwa.
Vuta picha ya maana hii kwa moyo wako ili umuombe usimamizi Mwenyezi Mungu na kupatia katika mambo yako, ili yale unayoyanuia katika hilo yawe katika mfano wa namna unavyofanya mshale.