عَنْ مُعَاوِيَةَ الْقُشَيْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ:
قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، مَا حَقُّ زَوْجَةِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ؟، قَالَ: «أَنْ تُطْعِمَهَا إِذَا طَعِمْتَ، وَتَكْسُوَهَا إِذَا اكْتَسَيْتَ، أَوِ اكْتَسَبْتَ، وَلَا تَضْرِبِ الْوَجْهَ، وَلَا تُقَبِّحْ، وَلَا تَهْجُرْ إِلَّا فِي الْبَيْتِ»
[حسن] - [رواه أبو داود وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 2142]
المزيــد ...
Kutoka kwa Muawia Al-Qushairi radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni zipi haki za mke wa mmoja wetu juu yake?, Akasema: "Ni umlishe pale unapokula, na umvishe unapovaa, au utakapopata kipato, na wala usipige uso, na wala usitoe maneno machafu, na wala usihame isipokuwa ndani ya nyumba".
[Ni nzuri] - - [سنن أبي داود - 2142]
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni zipi haki za mke juu ya mume wake? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akataja mambo kadhaa, miongoni mwa hayo ni:
La kwanza: Usijipendelee kwa chakula ukamuacha yeye; bali umlishe kama ulivyo kula wewe.
La pili: Usijipendelee kwa mavazi mazuri, bali umvishe utakapovaa wewe, na ukipata kipato na ukaweza.
La tatu: Usipige ila kuwe na sababu na haja ya kufanya hivyo, na akihitaji kumpiga ima kwa kumuadabisha au kwa kuacha kwake mambo ya faradhi, basi kiwe ni kipigo kisichovunja wala kujeruhi; na uso haupigwi;kwa sababu uso ndio kiungo kitukufu zaidi na kilicho wazi zaidi na kimekusanya viungo vitukufu, na viungo laini.
La nne: Usitukane au kusema: Mwenyezi Mungu auchafue uso wako; usimnasibishe yeye wala chochote katika mwili wake na ubaya ambao ni kinyume na uzuri; kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye aliutengeneza uso wa mwanadamu na mwili wake, na akakipa umbile zuri kila kiumbe, na kutukana umbile kunarudi katika kumtukana muumbaji, Mwenyezi Mungu atuepushe na hilo.
La tano: Usihame ila kitandani, na wala usiondoke hapo, na wala usimhamishie katika nyumba nyingine; na huenda hilo ni katika mambo yaliyozoeleka kutokea baina ya wanandoa.