عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ كَانَتْ لَهُ امْرَأَتَانِ فَمَالَ إِلَى إِحْدَاهُمَا، جَاءَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَشِقُّهُ مَائِلٌ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن أبي داود: 2133]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayekuwa na wake wawili akaegemea kwa mmoja wao atakuja siku ya Kiyama upande wake mmoja ukiwa umepinda".
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 2133]
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekuwa na mke zaidi ya mmoja, akawa hakufanya uadilifu baina ya wake zake uadilifu unaowezekana, ikiwemo kuwafanyia usawa katika matumizi na makazi na mavazi na malazi, nikuwa adhabu yake siku ya Kiyama nusu ya mwili wake itakuwa imepinda, na kupinda kwake ni adhabu kwake kwa sababu ya dhulma yake, kama alivyopinda katika muamala wake.