عن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إذا أَكَلَ أحدُكم فَلْيَأْكُلْ بِيَمِينِه، وإذا شَرِب فَلْيَشْرَبْ بِيَمِينِه فإنَّ الشيطان يأكلُ بِشِمَالِه، ويَشْرَب بِشِمَالِه».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Bin Omar Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Yakwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani shetani anakula kwa mkono wako wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Hadithi hii ndani yake kuna amri ya kula kwa mkono wa kulia, na kunywa kwa mkono wa kulia; na katazo la kula na kunywa kwa mkono wa kushoto, na kumebainishwa sababu ya hukumu hii, nayo nikuwa shetani anakula na kunywa kwa mkono wake wa kushoto, na inaonyesha pia kuwa amri hapa ni ya kuwajibisha, nakuwa kula na kunywa kwa mkono wa kushoto ni haramu, kwasababu yeye katoa sababu kuwa hicho ni kitendo cha shetani na ni tabia yake, na muislamu ameamrishwa kujiepusha na njia za watu waovu, achilia mbali shetani, na atakayejifananisha na watu fulani basi na yeye ni miongoni mwao.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kichina Kifursi Kihindi Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Ulazima wa kula na kunywa kwa mkono wa kulia, nakuwa amri katika hadithi ni ya kuwajibisha.
  2. Uharamu wa kula na kunywa kwa mkono wa kushoto.
  3. Kuna ishara kuwa ni lazima kujiepusha na matendo ambayo yanafanana na matendo ya shetani.
  4. Nikuwa shetani ana mikono miwili na kuwa yeye anakula na anakunywa.
  5. Kuutukuza mkono wa kulia; kwasababu sisi tumeamrisha tuutumie katika kula, na inafahamika kuwa kula ni lishe ya mwili, na matendo mema huwa kwa mkono wa kulia.
  6. Katazo la kujifananisha na makafiri; kwasababu sisi tumekatazwa kujifananisha na shetani, na shetani ndiye kichwa cha ukafiri.
  7. Nasaha za Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake, kwa umma pale alipowaelekeza katika jambo hili ambalo limefichikana kwao.